Saturday, October 3, 2009

TANGAZO
Timu ya soka ya LIPULI FC mkoani Iringa leo inashuka dimbani ktk uwanja wa Samora ktk mchezo wa kirafiki kukipiga na timu ya kurugenzi kutoka mjini Mafinga.
PAMBANO KATI YA TIMU YA SOKA YA LIPULI FC NA SIMBA FC MKOANI IRINGA KTK PICHA
Umati wa mashabiki wa Simba na Lipuli ukiwa ndani ya uwanja wa samora kabla ya mchezo wa kifariki kati ya Simba na Lipuli kuanza.
Wachezaji wa Simba wakisindikizwa na FFU baada ya mchezo kumalizika


Hivi ndivyo Ulinzi mkali ulivyo kuwa wakati wa mchezo kati ya Simba na Lipuli Fc Iringa katika mchezo wake leo Samora

Mchezaji wa timu ya Simba Davis Naftari akisaidiwa kupatiwa huduma ya kwanza katika lango la timu ya Lipuli Iringa siku timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa samora Iringa baada ya kugongana vichwa na mchezaji wa Lipuli Victor Jimmy ambapo wachezaji hao wote wawili walijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa ambapo mchezaji wa Simba alishonwa nyusi sita na mchezaji wa Lipuli alishonwa nyuzi 4,katika mchezo huo wa kirafiki Simba ilishinda kwa goli 1-0

Kocha msaidizi wa Simba Amri Said (kulia) akiwasindikiza wachezaji wa Lipuli na Simba walioumizana uwanjani leo ,

Mchezaji wa Lipuli Victor Jammy akiwa na jeraha kichwani ambapo lilimpelekea kushonwa nyuzi nne baada ya kugongana vichwa kwa bahati mbaya wakati akijaribu kuokoa mpira huku mchezaji Davis Naftari akijaribu kufunga goli bila mafanikio wachezaji wote wawili waliumia na kukimbizwa hospitali ya mkoa.